Internet de las cosas (IOT)
Intaneti ya Mambo ni dhana mpya iliyojikita katika muunganiko baina ya vifaa na kutengeneza mtandao kamili wa mawasiliano, ulio fanisi na wa kasi. Kimsingi inafanya kazi juu ya misingi ya teknolojia za ukusanyaji wa taarifa kama vile vihisio na mitandao ya mawasiliano kwa ajili ya mawasiliano ya hapo kwa papo kati ya vifaa vilivyounganishwa.
Kutokana na mifumo iliyotengenezwa chini ya mwamvuli wa IOT, muunganiko wa hali ya juu umeweza kufanikiwa, jambo ambalo linasababisha ufanisi katika ngazi zote. Ukusanyaji wa taarifa kupitia vihisio unawezesha utazamaji wa moja kwa moja, utumiaji kikamilifu wa muda na nafasi, pamoja na uwezo wa kuchukua hatua kulingana na kichocheo. Nyongeza, taarifa zote hizi zilizokusanywa ni muhimu ili kukuza taarifa kubwa na mifumo endeshi ya akili bandia, inayoweza kujifunza na kutabiri matukio ya mbele.
Muunganiko mkubwa wa IOT unawezesha mtiririko wa kiasi kikubwa cha taarifa kati ya vitu, vifaa na watu. Hii inawezesha uwezekano wa kubadilisha miji kuwa miji janja kwa kuunganisha karibu kila kifaa.
Kuna matumizi mengi: Ndani ya miji, inawezesha uangalizi wa kujiendesha wenyewe, usiobadilika wa wakati huo huo wa mabadiliko mbalimbali katika mazingira kama vile joto, unyevunyevu, upepo, miale ya jua, mvua, hewa na kiwango cha uchafuzi wa maji, kiwango cha pH ya maji n.k; mabadiliko yanayohusiana na mtembea kwa miguu na magari, ambayo ni muhimu katika usimamiaji wa msongamano na usafiri kwa ujumla. Nyanja nyingine ya muhimu ni ulinzi, sio tu kwa kutazma mifumo kwa kupitia kamera zilizofungwa katika maeneo muhimu, lakini pia kupitia utambuzi wa mpangilio wa baadhi ya watu na magari.
Wigo wa matumizi ya IOT ni mpana sana na hayajajikita mijini tu. Kilimo, uzalishaji, na maeneo maalumu kama vile katika afya yanafaidika nayo, hivyo kusaidia katika kujiendesha kwa shughuli mbalimbali.