Taa za sola
Taa za Betri za Miale ya Jua ni muunganiko wa teknolojia ya kuzalisha umeme kwa betri za miale ya jua (photovoltaic), hifadhi ya nishati, na taa za LED kwa pamoja. Kama taa za LED zimeleta mabadiliko makubwa katika upande wa taa za maeneo ya umma, basi taa za betri za miale ya jua ni zinaweka misingi ya mabadiliko yanayokuja mbele.
Moja ya suluhisho linalotumika mara kwa mara na lililofanikiwa katika Uwashaji wa Taa Janja kufikia mahitaji ya mwanga yanayohitajika ni taa za sola. Hizi ni muunganiko wa teknolojia kubwa tatu kama vile betri za miale ya jua, uhifadhi wa nishati na taa za LED, vyote ndani ya bidhaa moja.
Katika uwashaji wa taa za sola, bidhaa za kuonyesha ni aina ya taa zenye mjumuiko, tukimaanisha, zinakuwa na vitu vyote ndani ya kifaa kimoja. Upande wa juu kuna paneli za sola ambazo zinafyonza nguvu ya jua muda wa mchana, ambayo inahifadhiwa katika betri, ili mwisho iweze kutumika kuwasha taa za LED.
Moja ya vipengele muhimu zaidi vya kuangalia katika teknolojia hii ni betri: NextCity Labs® inatumia betri za viwango vya juu zenye teknolojia ya lithium iron phosphate (LiFePO4). Aina hii ya betri inaongoza kutumika hivi sasa katika kuhifadhi umeme kwa sababu ya usalama wake, ufanisi mkubwa haswa katika mazingira yenye joto, na uwezo wake wa kudumu. Betri yenye ubora itakuhakikishia kwamba bidhaa ina ubora na inatumika kwa muda mrefu kama ilivyotarajiwa.
Uwezo wa kujiendesha kwa betri ni jambo la muhimu sana kwa maendeleo ya miradi hii, hivyo inabidi ipangiliwe kwa namna tofauti kwa kila mradi, na mara zote zikisimamiwa na wataalamu waliobobea. Sababu ya tafiti zilizofanywa na timu nzima ya wahandisi wa NextCity Labs®, taa zinaweza kufungwa mijini na maeneo mengine ili kuzipa manispaa mbalimbali amani na uhakika wa mwanga kuwepo kila siku usiku mwaka mzima.
Ufanisi wa mwanga (Luminous efficacy) ni kipengele kingine cha ufungaji taa, haswa taa za betri za miale ya jua. Kiwango kikubwa cha ufanisi wa mwanga kitawezesha kumulika mwanga mkali kwa kutumia nishati kidogo, hivyo kuchangia katika kurefusha maisha ya betri.
Katika nyanja za kimazingira, uwashaji wa taa zinazotumia teknolojia ya betri za miale yajua kunawezesha matumizi ya taa yanayotokana na 100% ya nishati mbadala, kwa kutumia nishati inayotokana na betri za miale ya jua inapunguza nyayo za kaboni kwa kiwango cha chini kabisa. Kwa sababu hazihitaji kuunganishwa katika chanzo kikuu cha umeme, pia ni chaguo sahihi kwa maeneo yaliyo mbali kufikika yasiyo na miundombinu ya umeme au sehemu ambapo umeme hukatika mara kwa mara.
Gharama za kufunga taa hizi ziko chini sana, kwa sababu zinaondoa za umeme na gharama za kufunga nyaya. Unachofanya pekee ni kufunga taa mahali penye mwanga mzuri wa jua na utakuwa na mwanga wa kutosha wakati wa usiku.
Faida zake kwa jamii ni nyingi, hasa kama tukiangalia namna gharama za umeme katika manispaa mbalimbali zilivyo juu kila mwaka. Fedha hizi zinazookolewa zinaweza kutumika katika matumizi mengine muhimu ya kijamii kama vile katika afya. Ni muhimu pia kusisitiza umuhimu wa akiba hii ya nishati katika ngazi ya kidunia, ukizingatia kwamba taa za mijini zinachangia takribani moja ya tano ya matumizi ya umeme duniani.