Kampuni

Malengo yetu makuu ni kuifanya dunia yetu iwe mahali endelevu na kuboresha ubora wa maisha ya watu.

Play Video

NextCity Labs

Mapenzi na teknolojia

Sisi ni kampuni ya teknolojia ya Kihispania ya kimataifa, tupo Mexico, Chile na Hong Kong, na katika nchi nyingi pia kwa kupitia wasambazaji waliothibitishwa. Tunatengeneza na kuzalisha vifaa/suluhishi ya nishati mbadala katika miji janja. Bidhaa zetu zinapatikana katika masoko yenye uhitaji mkubwa duniani, ikiwa ni masoko katika mabara ya Ulaya na Marekani ambapo ndipo masoko yetu makuu yalipo.

NextCity Labs kama kampuni

NextCity Labs® ilitengenezwa katika misingi ya “Miji Janja”. Harakati zao wakizilenga katika kutumia uwezo mkubwa wa teknolojia na ubuniu, pamoja na rasilimali zingine, ili kupata ufanisi mkubwa, kutangaza uzalishaji endelevu na kuboresha ubora wa maisha ya watu. Kwa maana hii, tunaweka teknolojia zote hizi kwa ajili ya kuhudumia jamii na kubadilisha miji ya kawaida kuwa miji janja.

Ndani ya “Miji janja”, tumebobea katika nishati, eneo la kimkakati kwa kila namna, zaidi tukijikita katika: betri za kuzalisha umeme kwa miale ya jua (photovoltaics), uhifadhi wa nishati, kuhisi na IOT (Internet of things).

Sisi ni viongozi katika uvumbuzi unaounganisha teknolojia za viwango vya juu, kuzifunga katika vifaa vya kipekee kwa ajili ya mahitaji ya kampuni zetu, na siku zote tukijiamini na kutumia bidhaa zenye ubora na ustahimilivu, huku tukiweka miundo ya kuvutia katika kila bidhaa.

Maadili ya Kampuni

Mazingira

Mazingira ni msingi mkuu wa kampuni; tunatoa suluhisho mbalimbali kwa matatizo ya leo ili vizazi vijavyo viwe na ulimwengu mzuri zaidi.

Watu

Watu ni nafsi ya mji. Malengo ya ukuaji wowote wa teknolojia ni kuboresha ubora wa maisha ya watu.

Bidhaa zenye Ubora

Ubora wa bidhaa na zinazokidhi vigezo vya juu vya kiufundi. Vyeti vyetu vya uthibitisho vimetolewa kutoka katika mashirika makubwa ya kimataifa.

Imani na uaminifu

Matokeo ya bidhaa bora ni imani ya mteja. Pia tuna huduma kamili za baada ya mauzo ili kudumisha imani hiyo.

Kubadilika

Siku zote kusonga mbele katika kuboresha kampuni, bidhaa, na michakato yetu. Tunahudumia masoko ya duniani kote, na tuna wafanyakazi waliobobea kibiashara kwa ajili ya kuhudumia wateja na washirika wetu kwa lugha zao mama.

Utaalamu

Kampuni yetu imejikita katika eneo letu na tuna timu ya watu wa taaluma mbalimbali wenye ujuzi tofauti tofauti, wakitoa ujuzi, uzoefu wao na zaidi ya yote vipaji vyao.

“Miji ya siku za mbeleni ni lazima ijengwe kwa kuweka watu na mazingira mbele, kwa kutumia teknolojia ili kuwahudumia.”